Pages

Powered by Blogger.

Wednesday, April 1, 2020

MASWALI YA RIWAYA CHOZI LA HERI (ASSUMPTA K. MATEI)



TO GET ANSWERS TO ALL THIS QUESTIONS


Text Chozi to this no: 0711 224 186 together with your email  address or Whatsaap Number
The Answers will be sent to you after payment of 100/= to this Number 
0711 224 186


MASWALI YA INSHA
1) Eleza ufaafu wa anwani Chozi la Heri (ala20)
2) Kwa kurejelea kila sura onyesha jinsi mwandishi alivyoisuka kazi yake kufanikisha mtiririko na muumano wa vitushi.
3) Athari ya vita katika nchi ya Wafidhina ni kioo cha bara la Afrika. Jadili (ala 20)
4) Jadili dhana ya chozi katika riwaya ya Chozi la Heri (ala20)
5) Mwanamke katika jamii hii ametwezwa na kutwazwa jadili ( ala20)
6) Akikosa la mama hata la mbwa huamwa kwa kurejelea methali hii eleza umuhimu wa mashirika ya misaada (ala20)
7) Jamii ya Chozi la Heri ni taswira ya jinsi ukabila unavyoathiri bara la Afrika (ala20)
8) Malezi ya watoto katika riwaya ya Chozi la Heri ndicho kitovu cha ufanisi na matatizo yote yanayowapiku watoto (ala20)

9) Utumizi wa afyuni katika jamii umeleta mathara mengi . Thibitisha (ala 20)
10) Jadili athari na dhiki zinazotokana na uongozi mbaya (ala 20)
11) Mla, naye huliwa zamu yake ikifika . kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri thibitisha ukweli wa kauli hiyo (ala 20)
12) Riwaya ya Chozi la Heri imejaa aina mbalimbali za migogoro jadili. (ala 20)
13) Uozo wa maadili na kuvunjwa kwa haki ni jambo ambalo lilikuwa la kawaida katika nchi ya Wahafidhina. Thibitisha (ala20)
14) Riwaya ya Chozi la Heri ni ya Utamaushi jadili kauli hii (ala20)

MASWALI YA MUKTADHA
Weka dondoo hizi katika muktadha wake
1) “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa”
2) “ Usiku umekuwa mpevu, twende tusije tukamtia mama kiwewe’’
3) “ Huenda nikapata mbinu ya kujinasua baadaye’’
4) “ Di, usijali. Mimi nitawakimu kwa viganja hivi vyangu. Hamtapungukiwa na lolote’’
5) “Basi Doc, nakubaliana na rai yako”
6) “ Huyu hapa ameletwa na wasamaria wema leo asubuhi’’
7) “ Je ni yule aliyeletwa jana usiku wa kuamkia jana’’
8) “ Hatuwezi kumkabidhi mzee wetu huyu kifaranga kitekite hivi, tutakuwa tunampagaza uzazi”
9) “ Yako ya arubaini imefika”
10) “ Wenye hadhi na mali wanahitaji wafanyikazi wa kuwaendelezea biashara zao’’
11) “ Usiwe na mawazo finyu na hasi kuhusu kumpanga mtoto’’
12) “ Karibuni naona mmetuletea kilaika’’
13) “ Tulipata ombi lenu kuhusiana na suala la kumpanga mojawapo wa watoto wetu’’
14) “ Ndugu zako wako hai na bila shaka mtakutana”
15) Yote haya yamewezekana kutokana na mwongozo mlionipa nyinyi. Zaidi , utulivu nilioupata nilipoambulia familia hii ulinipa msukumo kila mara nilipokabiliwa na ndaro
16) “ Njoo nikujuze kwa yule binamu vuuk ambaye hukwambia habari yake kila mara”
17) “ Atanguliaje kisimani hunywa maji maenge”
18) “ Mlaani shetani”
19) “ Huyu ana imani”
20) “ Umu hawa ni marafiki wangu wa chanda na pete. Ni watu wakarimu na wenye imani’’
21) “ Nashukuru kwa kunielekeza kwa wazazi wetu hawa”
22) Wote wawili walitazamana, kila mmoja akiapa moyoni kuwa amewahi kumwona kiumbe huyu mahali.
23) Kweli mimi nilikuwa sikio la mbuzi ambalo nyanya alizoea kusema husikia chunguni
24) “ Leo waonaje tukiwajaribu mababe wetu? Ni vizuri kuanza mapema kabla ya jua la utosini”
25) “ Mama zenu walienda wapi?”
26) “ peace be with you’’
27) “ Kweli milima ndiyo haikutani”
28) “ Nahisi kama nasimulia kisa kirefu chenye mwisho mwema”
29) “ Si kwamba sijawatafuta hamna kituo cha polisi ambacho sijabisha hodi”
30) “ Haiwezekani! Hili haliwezekani! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”
MASWALI YA WAHUSIKA NA UHUSIKA
Jadili sifa za wahusika wafuato na umuhimu wao katika Riwaya;
• Ridhaa
• Mwangeka
• Mwangemi
• Umulkheri
• Lunga
• Bwana Kaizari
• Mwekevu
• Mzee Mwimo msubili
• Tila
• Kairu
• Zohali
• Mwanaheri
• Chandachema
• Neema
• Sauna
• Pete
• Mwaliko
• Mwalimu Dhahabu
• Dickson
• Bwana Maya
• Naomi
• Mzee Kedi
• Hazina
MASWALI YA MBINU ZA LUGHA (FANI NA MTINDO) PAMOJA NA TAMATHALI ZA USEMI
Jadili mbinu zifuatazo zilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri:
Ø Jazanda
Ø Taharuki
Ø Barua
Ø Ndoto
Ø Kinaya
Ø Taswira
Ø Sadfa
Ø Majazi
Ø Mbinu
rejeshi
Ø Maswali balagha

0 comments:

Post a Comment