Huku ukirejelea
hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji
wa haki.
TUMBO LISILOSHIBA.
(i)
Viongozi
kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao.
(ii) Kutowahusisha maskini
katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
(iii)
Kunyakua
ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.
(iv) Kupanga njama
za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.
(v) Jitu la miraba
mine kula chakula chote bila kubakishia wateja.
(vi) Wanamadongoporomoka
kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
(vii)
Askari
wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa .
(viii)
Jeshi
la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa vibanda vya wanamadongoporomoka.
ix) Askari kuwapiga virungu watu.
SHIBE INATUMALIZA.
(i)
Mzee
mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
(ii) Waajiriwa
kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
(iii)
Viongozi
kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
(iv) Waajiriwa
wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura ni mawaziri wa wizara moja.
(v) Mzee mambo
kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari kwa kutumia pesa za umma.
(vi) Mzee mambo
kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali za nchi- magari, vyakula.
(vii)
Sasa
na mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.
0 comments:
Post a Comment