Majina mengi ya wahusika yamejengwa kimajazi ambapo
majina hayo yamebeba tabia za mhusika mwenyewe.
Ridhaa;
jina
hili linabeba maana ya hali ya kukubali au kutosheka na jambo Fulani. Mhusika
Ridhaa anakubaliana na hali ya upweke uliomkuta baada ya kufiwa mkewe
Terry,mwanawe Tila,mkaza mwana wake Lily na mjukuu wake Beky. Katika
kukubaliana na hali hiyo,Ridhaa anaacha kundoa majivu ya miili hiyo iliyotekea
kwa moto ili kukubaliana na hali hiyo
Tenge;
jina
hili linarejelea kwenda kombo. Kitendo cha Bwana huyu hususan kitendo kitendo
cha kuigiza wanawake ndani na kushiriki nao ufuska wakati mkewe ameenda kazini
kinasawiri kabisa jina lake.
Wahafidhina;
hili nalo ni jina la kimajazi likiirejelea jamii isiyotaka kubadili mtazamo wa
mambo .Mwandishi ametumia jinahilo kwa kuwakatika jamii bado kuna watu
wameshikilia msimamo kwamba mwanamke hawezi kupewa madaraka ya juu ya
kiuongozi.
Msitu
wa Heri; hii ni ardhi
iliyokuwans rutuba.Bwana Lunga-Kiriri Kangata aliweka makazi yake hapa
akajikuta heri imemwangujia kutokana na kufaidi mazo ya kilimo. Hata
hivyo,kitumbua kiliingia mchanga walipofurushwa na dola kwamba wanaishi hapo
kiharamu.
Mwekevu
Tendakazi; jina Mwekevu limetokana na nenola Kiswahili
“wekeza” lenye maana ya kufanya jambo Fulani kwa lengo la kuzalisha Zaidi
baadaye.Jina Tendakazi ni mwambatano wa manen “tenda” na “kazi” kwa maana ya
kufanya shughuli. Mwekevu Tendakazi aliweka juhudi nyingi katika kuwainua raia
alipokuwa mkurugenzi wa Shirika la Chemchemi ambazobaadaye zlizaa matunda kwa
wnanchi kumwamini na kumchagua
Majina mengine ya kimajazi ni kama vile
Dhahabu,Mwenge,Chandachema,Hazina,Waridi,Subira,Neema,Nyangumi,Kipanga,Tindi.
Spelling error
ReplyDelete